Tetesi za soka kimataifa

 


Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, anafanya mazungumzo na DC United kuhusu kuhamia klabu hiyo ya Major League Marekani. (Football London)

Mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos, 34, amekataa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja na Real Madrid, ambayo haitaki kwenda kinyume na sera yao ya kutoa makubaliano zaidi ya 30 ya muda huo kwa wachezaji wake.

Real iko katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi wa Bayern Munich raia wa Austria David Alaba, ambaye hajakuwa kwenye mkataba wowote msimu huu lakini Liverpoolpia imeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, 28. (Guardian)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ana uhakika wa asilimia mia moja kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne atatia saini makubaliano mapya na klabu hiyo, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo, 29, amepanga kukataa ofa ya mkataba wao. (Sky Sports)

Arsenal imehusishwa na kiungo wa kati wa Norwich City Emi Buendia lakini kuna uwezekano mdogo sana ikamsajili raia huyo wa Argentina, 24, kwasababu ya ukosefu wa pesa. (Mirror)

Tottenham Hotspur imesitisha mazungumzo na washambuliaji wa England Harry Kane, 27, na yule wa Korea Kusini Son Heung-min, 28, kutokana na janga la virusi vya corona. (Evening Standard)

nsa Kingsley Coman amehusishwa na Manchester City na Manchester United lakini mchezaji huyo, 24, anasema " yuko sawa na mwenye furaha" Bayern Munich. (Bild, via Mirror)

West Ham United huenda ikaanza kutafuta mbinu za kumsajili mshambuliaji wa Italia Graziano Pelle, ambaye tu ndio ameondoka klabu ya Shandong Luneng ya Chinese Super League ikiwa itashindwa kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28. (Star)

Hammers imeamua kutomsajili mshambuliaji wa Austria, 31, Marko Arnautovic, aliyehama klabu hiyo na kujiunga na Shanghai SIPG ya Chinese Super League kwasababu itakuwa gharama sana kwao. (Mail)

Kiungo wa kati wa Real Madrid, 24, Dani Ceballos, ambaye yuko Arsenal kwa mkopo ana matumaini ya kurejea kwa klabu yake ya utotoni na kushiriki katika kikosi . (Cadena Ser, via Evening Standard)

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman anasema ametengeneza orodha ya wachezaji "ambao itakuwa bora wakipatikana". (Marca)

Brentford inamnyatia kiungo wa kati wa Preston North End Ben Pearson, 26, ambaye mkataba wake na klabu ya Deepdale unakamilika msimu huu. West Bromwich Albion na Celtic pia zimehusishwa na mchezaji huyo. (Mail)

Aliyekuwa mshambuliaji wa England na Southampton James Beattie ni miongoni mwa wagombea wanaopigania kuchukua nafasi ya kocha wa timu ya Fleetwood Town baada ya Joey Barton kuondoka. (Mail)


Tetesi za soka kimataifa Tetesi za soka kimataifa Reviewed by cmakigo on January 06, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.