Kiungo wa Tottenham na England Dele Alli, 24, "anataka" kuhamia klabu bingwa ya Ufara Paris St-Germain Lakini mazungumzo baina ya timu hizo yamekuwa magumu. (Mwandishi Fabrizio Romano, kupitia Twitter)
Klabu ya West Ham United inapima uwezekano wa kumsajili mshambuliaji kutoka Ufaransa Gaetan Laborde, 26, ambaye ka sasa anachezea klabu ya Montpellier. (Telegraph )
gracia
Kaimu rais wa Barcelona Carles Tusquets amependekeza kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20, kwa euro milioni 8 kwa wagombea watatu wa urais wa klabu hiyo, lakini hakuna kinachoweza kufanyika kwa sasa kwa kuwa wote hakuwa na makubaliano. (Marca)
Mshambuliaji wa Uholanzi Netherlands Memphis Depay, 26, anasema yeye na mchezaji mwenzie wa klabu ya Lyon Houssem Aouar, 22, wanataka kuhamia katika "moja ya klabu tatu kubwa duniani." Depay amekuwa akihusishwa na klabu ya Barcelona, huku kiungo kutoka Ufaransa Aouar anaripotiwa kunyemelewa na Arsenal. (Canal+)
Kocha wa Fulham Scott Parker anasema anataka kusajili wachezaji na kumaliza biashara ya usajili mapema katika dirisha la mwezi huu. (Evening Standard)
morgan
Kocha wa Marseille Andre Villas-Boas amethibitisha kuwa kiungo Mfaransa Morgan Sanson, 26, ananyemelewa na klabu kadhaa za England zikiwemo; Arsenal, Aston Villa, Tottenham na West Ham.(Mail)
Mkurugenzi wa Inter Milan Beppe Marotta amesema kuwa klabu hiyo ipo vizuri kifedha lakini haitafanya uwekezaji wowote wa wachezaji katika dirisha la usajili la mwezi huu. (Sky Sport Italia)
Kocha wa Hull City Grant McCann ametangaza kuwa mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Keane Lewis-Potter, 19, hauzwi, japo mazungumzo juu ya mkataba mpya baina ya Hull na mchezaji huyo yanaelekea Lugongo mwamba. (Yorkshire Post)
No comments:
Post a Comment