Yajue madhara yatokanayo na kusikiliza mziki kwa kutumia spika za maskioni ( earphone & headphone)

 


Katika kizazi hiki cha burudani kumezuka tabia ya watu kutumia vitu vya kisasa katika ku sikiliza muziki ili kuepuka kuwabugudhi watu wengine., na watu hao wamekuwa wakitumia vitu kama earphone au headphone kuweza kusikiliza muziki huo.


Ila ukweli ni kwamba kusikiliza mziki kwa sauti ya juu kwa kutumia spika za masikioni (earphones & headphones) zaweza kutuweka katika hatari ya kupata uziwi.


Spika za masikioni zimetengenezwa ili kumuwezesha mtumiaji kusikiliza sauti kutoka katika kifaa chake wakati wowote atakapohitaji na hata kama amezungukwa na mazingira yenye kelele.


Usikilizaji wa sauti ya juu au sauti kubwa kwa kutumia spika za masikioni kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata uziwi pia hata uziwi wa moja kwa moja. Usikilizaji huu wa sauti kubwa ni hatari zaidi kwa watoto na vijana kwa kuwa hupendelea kusikiliza muziki kwa sauti ya juu aidha nyumbani au katika vilabu vya muziki, kwenye magari na hata kwa kutumia spika za masikioni.


Sauti hupimwa kwa kutumia skeli ijulikanayo kama decibel (dB).Mfano mtu anayeongea kwa sauti ya chini ni kadirio la 30 dB.


Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), kupitia takwimu zilizopatikana katika nchi zenye kipato cha kati zinaonyesha kuwa, miongoni mwa wale walio na umri kati ya miaka 13-35,karibu asilimia 50 husikiliza sauti katika kiwango kisicho salama kwa kutumia vifaa vyao binafsi vya sauti na asilimia 40 huwa katika kiwango kisicho salama cha sauti wakiwa katika kumbi za starehe.


Shirika la afya (WHO) limeainisha kuwa, kukaa eneo lenye kiwango cha sauti kuanzia 85dB kwa masaa nane au 100dB kwa dakika 15 kuwa siyo salama. Inakadiriwa kuwa 1.1bilioni ya walio chini ya miaka ishirini(teenagers) na vijana wako katika hatari ya kupoteza usikivu kutokana na matumizi ya vifaa vya sauti zikiwemo simu za mkononi(smartphones) zinazoambatana na spika za masikioni.


Kusikiliza isivyo salama itategemea kiwango cha sauti, muda ambao utasikiliza na ni mara ngapi unasikiliza.


Inashauriwa kuwa kiwango cha juu cha sauti katika maeneo ya kazi ni 85dB na isizidi masaa nane kwa siku. Wafanyakazi wa vilabu vya usiku na baa mara nyingi huwa katika kiwango cha juu cha sauti na wanashauriwa kupunguza masaa ya kazi. Kwa mfano katika klabu za usiku, huwa na kiwango cha 100dB kwa hiyo itakuwa salama kwa masikio yetu endapo tutakaa katika kumbi hizo kwa dakika 15 tu.


Walio chini ya umri wa miaka ishirini na vijana waweza kujilinda kwa kuweka tuni za chini katika vifaa vyao vya sauti au kuvaa vifaa vya kuzuia sauti wawapo maeneo yenye sauti kubwa ili kuepuka kupata uziwi. Pia waweza kupunguza muda watakaokaa katika eneo lenye sauti kubwa au kuepuka matumizi ya mara kwa mara au siku chache za kutumia vifaa vya sauti kama spika za masikioni.


Yajue madhara yatokanayo na kusikiliza mziki kwa kutumia spika za maskioni ( earphone & headphone) Yajue madhara yatokanayo na kusikiliza mziki kwa kutumia spika za maskioni ( earphone & headphone) Reviewed by cmakigo on January 18, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.