Mahakama ya Misri imechukuwa uamuzi wa kuhamisha mali za wanachama 89 wa Ikhwan (Muslim Brotherhood) kwa hazina ya serikali.
Kulingana na taarifa za gazeti linalomilikiwa na serikali Ahbar al-Yawm, Mahakama ya Ushuru ya Cairo ilifungua kesi iliyoletwa na Tume ya Unyakuzi wa Mali za Ikhwan na kutoa uamuzi wa kuchukuliwa kwa mali za watu 89 wakiwemo warithi wa mali za kiongozi wa Ikhwan Rais wa zamani Mohammed Morsi aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza ambao ni mkewe pamoja na watoto wake.
Kamati hi
Ilielezwa kuwa uamuzi wa mahakama ulihusisha mali za mke wa Morsi Najla Ali Mahmud na watoto wao Ahmed, Sheima, Husame na Omar.
Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Kituo cha Vijana cha Haki za Kibinadamu, ambacho makao yake makuu yapo nje ya Misri, ilielezwa kuwa uamuzi huo ulichukuliwa kwa tuhuma za ushirika wa kigaidi na kulaani hatua hiyo ya unyang’anyi wa mali za raia kisiasa.
Baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Julai 2013, Ikhwan ilitangazwa kuwa kama shirika la kigaidi mnamo mwezi Desemba mwaka huo huo.
No comments:
Post a Comment