Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho.
Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako .Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma. Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo.
Tambua ya kuwa, "hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho". Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma.
Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati. "Habari njema ya siku ni leo, na siku nzuri yako ni ya kesho "
Ukiona umesononeka kwa maisha kuwa magumu jua unaumia kwaajili ya maisha yako ya nyuma, maana unawaza jinsi ulivyo shindwa kulipa kodi ya nyumba,ulivyoshindwa kulipa umeme, maji, ada za watoto na ulivyoshindwa kuendesha biashara yako au ulivyoshindwa kuitetea ajira yako. Usipoteze Muda wako kwa kuwaza yaliopita badala yake waza kesho yako itakuwaje.
Unawaza mahusiano ya nyuma yalivyokuumiza na kukutesa, ulivyosalitiwa na kuachwa, ulivyopewa mimba na kuachwa, ulivyomsomesha kisha akakutaaa, unawaza kias kwamba unashindwa kusonga mbele na maisha mapya, Unashindwa kuanzisha mahusiano mapya kwa sababu ya mjinga mmoja alaiyekuumiza?
Unajua yeye anayo furaha huko alipo na ww huku unatembea na past yake unampa ushindi kama ulikuwa haujui na anajipiga kifua kwa kusema hawez kumpata kama mimi ndiyo maana bado hana mtu? Huu ni utumwa na mateko wa moyo amka sasa ya nyuma yashatokea yachukue kama funzo. Mwisho wa siku maisha lazima yasonge mbele.
Waswahili wanasema yaliopita si ndwele, tugange yajayo. Huwezi kubadilisha jana, Bali waweza kubadilisha kesho yako kwa kufanya maamuzi leo. Usipoteze Muda kwa kugeuza shingo yako kutazama ya nyuma, utajikuta unadumbukia katika shimo la maisha magumu.
"You can't have a better tomorrow if you are thinking about yesterday all the time "
Busara yangu: Usikate tamaa, usivunjike moyo, usirudi nyuma, maisha lazima yaendelee... Sahau ya nyuma ione leo yako ni ya mhimu sana, yaliyokutokea jana yasikukatishe tamaa kamwe..
No comments:
Post a Comment