China imesema ingali inajadiliana na Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu tarehe na pia mipangilio kwa wataalamu wa kimataifa wanaochunguza chimbuko la virusi vya corona kuzuru nchi hiyo.
Hii ni baada ya mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus kuishutumu China kwa kushindwa kutoa vibali kwa wataalamu hao kuzuru China.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa China Hua Chunying amewaambia waandishi wa Habari mjini Beijing kwamba msimamo wa China kuhusu juhudi za kujua chanzo cha janga hilo zimekuwa wazi tangu mwanzo.
Ameongeza kuwa China inashirikiana kwa karibu na WHO, lakini tarehe na mipangilio ya juhudi hizo inapaswa kukamilishwa.
Mnamo Jumanne, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema wanasayansi wa timu ya kimataifa wanaotaka kuchunguza chimbuko la virusi hivyo wameanza safari kuelekea China lakini China haijafanikisha vibali vya wataalamu hao.
No comments:
Post a Comment