Shirika la ndege la Pegasus limetoa taarifa kuhusu kusimamishwa kwa muda kwa ndege kutoka Uingereza kwenda Uturuki.
Katika taarifa kutoka kwa akaunti za media ya kijamii ya kampuni hiyo, Uturuki imesimamisha safari zake kwa muda na Uingereza.
"Baada ya uamuzi wa mamlaka rasmi, kuanzia tarehe 2 Januari 2021, ni abiria tu wanaosafiri kuunganisha kwenda nchi nyingine (Transit) watakaokubaliwa.Abiria watakubaliwa katika ndege kulingana na sheria za nchi watakayokuwa wanaenda."
Katika taarifa yake jana jioni, Waziri wa Afya Fahrettin Koca alitangaza kwamba baada ya kugundulika kwa virusi vipya vya corona kwa watu 15 ambao waliingia nchini kutoka Uingereza hivi karibuni, safari zimesimamishwa kwa muda.
Shirika la Ndege la Pegasus lasitisha safari na Uingereza
Reviewed by cmakigo
on
January 03, 2021
Rating:

No comments:
Post a Comment