Mashindano ya netiboli yanayofanyika kitaifa mjini Babati mkoa wa Manyara yameanza rasmi leo Januari 3,2021 yakishirikisha timu kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Singe, Arusha waliwachakaza Simiyu mabao 69-12 huku mchezo wa pili wenyeji Manyara wakiifunga Tabora mabao 38-25.
Afisa michezo mkoa wa Manyara amesema michuano hiyo ni fursa kwa mkoa wa Manyara katika kuutangaza na kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na hatimaye mkoa.
Amesema michezo hii ikianzishwa kuanzia ngazi ya shule ya msingi itasaidia kutengeneza timu nzuri za mikoa na taifa kwa ujumla.
Amewataka wakazi wa mkoa wa Manyara kujitokeza kushangilia ili kuwatia moyo wachezaji.
Waamuzi waliochezesha michezo hiyo ni Beatrice kutoka Morogoro, Masumbuko kutoka Mwanza na Constancia Kisege kutoka Simiyu, daktari wa wachezaji ni Dr.Joseph Sanga kutoka hospitali ya mji wa Babati Manyara.

No comments:
Post a Comment