Ijue Asili Ya Tanzania Kiundani Zaidi

 


Kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani


Jina "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar (pamoja na athira ya jina la kale la "Azania").


Nchi hizo mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa makoloni ya kawaida.


Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza).


Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.


Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais.


Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani.


Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa.


Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa.

Tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata miundo ifuatayo:


Nchi inatawaliwa na serikali ya muungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.

Tanganyika au Tanzania bara haina serikali wala bunge la pekee.

Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano.

Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za muungano:

Mambo ya nje

Jeshi

Polisi

Mamlaka ya dharura

Uraia

Uhamiaji

Biashara ya nje

Utumishi wa umma

Kodi ya mapato, orodha

Bandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu

Demografia

Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kunaishi mtu mmoja tu kwenye kilomita moja ya mraba (1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba.

Makabila


Zaidi ya asilimia themanini huishi vijijinye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya, Wajaluo na Wamakonde.


Idadi kubwa sana ya Watanzania ni jamii ya Wabantu. Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome na Wasi. Kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina yao ni Wasandawe na Waburunge. Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati. Pia kuna asilimia ndogo ya watu wa asili nje ya bara la Afrika mfano Wahindi,Waarabu,Waindochina,Wafarsi,Wachina na Waingereza. Hii ilisababishwa kwa karne na karne za mchanganyiko wa mahitaji ya biashara yaliofanywa na mabara ya Ulaya na Asia hapo Afrika.


Lugha

Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya mia moja na ishirini. Hakuna lugha rasmi kisheria, lakini Kiswahili ndiyo lugha ya taifa.


Ingawa kila kabila lina lugha yake, lugha ya taifa ya Tanzania ni Kiswahili ambacho ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu. Hali hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.


Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo ya rasmi; kwa hiyo ni lugha rasmi ya dhati. Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari, na kwa hiyo ilichukuliwa kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi wa rasmi wa Kiingereza imepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati pekee.


Dini

Makala kuu ya: Dini nchini Tanzania

Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi inawezekana ni zaidi azimio la kisiasa.


Kwenye visiwa vya Zanzibar idadi ya Waislamu huaminiwa kuwa takriban 97%.


Usafiri

Habari za undani zaidi katika makala ya Usafiri wa Tanzania

Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Mengine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani la Bahari Hindi kuna pia usafiri kwa meli.


Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-madharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu.


Shirika mbili za reli zahudumia Tanzania ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali.


Huduma kwa ndege zatumia hasa nyanja za ndege 11 penye barabara ya lami kwa ajili ya ndege hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni.


Utamaduni na sanaa

Bombwe la Kimakonde: Tembo

Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.



Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.


Tangu miaka ya 1970 uchoraji wa "tingatinga" umejulikana: ulipata jina hilo kutoka kwa Edward Tingatinga naye mtu wa Umakonde.


Utamaduni wa Watanzania ni pamoja na utaraab. Muziki ana nyimbo za kitaraab ndizo muhimu sana kwa nchi nzima, hasa visiwani na pwani. Pia kuna miziki ya Kinyarwanda, dansi kama intore n.k.


Urithi wa Dunia


Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".


Mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali

1979 – Hifadhi ya Taifa Ngorongoro

1981 – Hifadhi ya Taifa la Serengeti

1981 – Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara

1982 – Hifadhi ya Taifa Selous

1987 – Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro

2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja

2006 - Michoro ya Kondoa


Ijue Asili Ya Tanzania Kiundani Zaidi Ijue Asili Ya Tanzania Kiundani Zaidi Reviewed by cmakigo on January 08, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.