Bobi Wine awapeleka watoto wake nje ya nchi akihofia usalama wao

 


Mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine amethibitisha kupeleka watoto wake nje ya nchi kwa kuhofia usalama wao.

Bobi Wine amesema taifa hilo linafahamu vyema changamoto ambazo familia yake imepitia tangu alipoamua kupambana na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu unaofanyika Januari 14.

‘’Watoto wangu wameishi kwa hofu kwa kipndi cha miaka mitatu iliyopita.

‘’ Mara nyingi tu gari linalotufuatilia limekuwa likiwafuatilia na wao hata kwenda na kutoka shuleni’’, amesema Bobi Wine.

Bobi Wine pia amesema kuwa mwaka jana, gari lililokuwa linasafirisha watoto wake lilishambuliwa moja kwa moja jambo lililomfanya kuwabadilisha shule na kuimarisha usalama wao.

Kulingana na Bobi Wine kwa kipindi kirefu mwaka huu, watoto wake wameishi kama wafungwa ikiwa ni nadra sana wao kutoka nje ya nyumba yao.

Katika akaunti ya mtandao wake wa Facebook, Bobi Wine amesema kuwa amepokea taarifa za mipango ya kuwadhuru watoto wake.

‘’Mwaka 2017, usiku wa mdahalo, walimrushia kijana wangu gurunedi, kupitia dirisha la chumba chake cha kulala na kuacha ujumbe kwamba nijiondoe au matokeo nitayaona’’, amesema Bobi Wine.

Na kuongeza kuwa hiyo ndio sababu alipopokea taarifa za njama ya kumvamia yeye, mke wake na kutekwa nyara kwa watoto wake, rafiki zake nje ya nchi wamejitolea kukaa na familia yake kwa muda.

‘’ Haimaanisha kuwa mimi na mke wangu tuko salama kwa kusalia nyuma. Lakini juhudi zetu ni kuhakikisha kuwa hawapati fursa ya kuteka nyara watoto wetu na kuitumia kama njia ya kunitisha’’.

Bobi Wine amesema katika nchi yenye demokrasia hakuna anayestahili kuishi kwa hofu kwasababu tu anapinga serikali.

‘’ Katika nchi iliyo huru, hakuna mgombea urais atakayevaa jaketi la kuzuia risasi na kofia ngumu (helmet) ili kwenda kufanya kampeni’’, amesema Bobi Wine.

Vilevile, Bobi Wine ameonesha kutoridhishwa na kitendo alichodai kuwa mfanyakazi wa uhamiaji amevujisha taarifa za watoto wake kusafiri nje ya nchi.


Bobi Wine awapeleka watoto wake nje ya nchi akihofia usalama wao  Bobi Wine awapeleka watoto wake nje ya nchi akihofia usalama wao Reviewed by cmakigo on January 07, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.