Mwenyekiti wa kampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, amepoteza kiasi cha dola milioni 900 katika hisa nchini Nigeria, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bloomberg.
Kwa mujibu wa jarida la Bloomberg, ambalo huripoti kuhusu watu 500 tajiri zaidi duniani, mapato ya Dangote yalishuka kwa kiwango cha dola bilioni 18.4 siku ya Alhamisi hadi dola bilioni 17.5 siku ya Ijumaa ,akishuka kutoka mtu wa 106 hadi hadi mtu wa 106 katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani , kulingana na gazeti la Punch.
Mwezi Disemba mwaka jana, utajiri wa Dangote ulikuwa na jumla ya thamani ya dola bilioni 17.8 kutoka dola bilioni 15.5 zilizoripotiwa awali.
Dangote alipata mapato ya ziada ya dola milioni 600 katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Januari 2021, lakini kapoteza pesa yote hiyo Ijumaa iliyopita.
Hata hivyo Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika na mtu mweusi tajiri zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment