Akaunti za Facebook zinazounga mkono chama cha Museveni zafungwa

 


Wafuasi wa rais Yoweri Museveni wamelalamikia kampuni ya Facebook kwa madai kuwa ilifunga akaunti zao kwenye mtandao huo.

Wamiliki wa akaunti 50 za Facebook zinazounga mkono chama tawala nchini Uganda cha National Resistance Movement [NRM] wamedai akaunti zao zilifungwa huku jumbe zao zikifutwa kabisa au kushidwa kuchapishwa kupitia mtandao huo wa kijamii.

“Aibu kwa mamlaka za kigeni ambazo zinadai zinaweza kupandikiza uongozi wanaoweza kuutumia kwa kuzuia utendaji wa akaunti za mtandao za wafuasi wa NRM . Hautamtoa RaisYoweri Kaguta Museveni,” alisema afisa wa habari wa rais Don Wanyama.

Mwanaboligi maarufu nchini Uganda Ashburg Kato alidai kuwa kampuni kubwa ya teknolojia yenye makao yake makuu California ilifuta akaunti zao kufuatia maombi ya chama tawala cha upinzani nchini Uganda cha National Unity Platform (NUP) cha mgombea Robert Kygulanyi al maarufu Bobi Wine na ''washirika '' wake

“Facebook yenyewe ilifuta akaunti zetu kutokana na ombi la washirika wa Bobi Wine''Kato alitweet.

Alitoa wito kwa rais achukue hatua dhidi ya Facebook.

Akaunti za Facebook zinazounga mkono chama cha Museveni zafungwa Akaunti za Facebook zinazounga mkono chama cha Museveni zafungwa Reviewed by cmakigo on January 11, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.