Virusi vya corona: Jinsi maradhi hayo yalivyovuruga sherehe za mwaka mpya duniani


Vizuizi vimewekwa dhidi ya sherehe za mwaka mpya katika maeneo tofauti duniana wakati nchi nyingi zinajizatiti kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya coronaona.
Onyesho la fataki na mikusanyiko ya watu ilipigwa marufuku kuanzia Sydney hadi New York.
Sherehe pia zimezimwa hususan barani Ulaya baada ya aina mpya ya ugonjwa ambao maambukizi yake yanasambaa kwa kasi kugunduliwa
Ufaransa iliweka zaidi ya polisi 100,000 kushika doria katika barabara za mji mkuu mkesha wa mwaka mpya ili kuhakikisha amri ya kutotoka nje nyakati za usiku zinazingatiwa.
Zaidi ya watu milioni 1.8 wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona tangu janga hilo lilipoanza mwaka mmoja uliopita.
Nchini Ufaransa, serikali iliamuru uwepo wa usalama katika maeneo ya mijini kutoka 20:00 (19:00 GMT) Alhamisi, wakati amri ya kutotoka nje ilipoanza.
Katika mji wa Paris nusu ya usafiri wa metro ilifungwa.
Ufaransa ilikuwa imeweka amri ya kutotoka nje huku mabaa, migahawa na maeneo ya vivutio vya watu yakisalia kufungwa walipokaribisha mwaka mpya
Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Rais Emmanuel Macron aliwaangazia wakosoaji wanaolalamikia kujikokota kwa mpango wa kutoa chanjo, na kuapa kushughulikia suala hilo katika "muda unaostahili".
Nchini Uingereza - ambako virusi vipya vya corona vinavyosambaa kwa kasi vimegunduliwa huku watu milioni 20 wakiathiriwa zaidi katika eneo hilo watu wamelazimika kusalia majumbani mwao - Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa wito wa watu kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Barabara za mji wa London zilikuwa kimya mkesha wa mwaka mpya baada ya polisi kuomba watu washerehekee majumbani mwao.
Badala ya sherehe za kawaida zinazojumuisha mikusanyiko ya watu jijini London, onyesho la fataki lilifanywa katika maeneo tofauti jijini humo.
Ireland iliongeza vikwazo zaidi siku ya Alhamisi, kwa kupiga marufuku watu kutembeleana majumbani na kufunga maduka ambayo hayauzi bidhaa muhimu na kudhibiti usafiri wa hadi kilomita 5.
Ujerumani kwanza sasa imeweka amri ya kutotoka nje hadi Januari 10. Serikali imepiga marufuku uuzaji wa fataki na kuweka vikwazo vikali vya kudhibiti idadi ya watu wanaokusanyika pamoja.
Katika hotuba yake ya mwaka mpya inayotazamiwa kuwa ya mwisho kwake kama kansela wa Ujerumani, Angela Merkel aliwaangazia watu wanaopotosha umma kuhusiana na janga hilo.
Alisema anashangazwa na jinsi uwongo wa kijinga na wa kikatili unavyotumiwa bila kujali hisia za wale waliyopoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa corona
Nchini Italia, amri ya kutotoka nje iliwekwa saa 22:00 huku mabaa, migahawa na maduka mengi kufungwa. Huku hayo yakijiri Papa Francis hakuongoza ibada ya mwaka mpya mjini Rome badala ya kupata maumivu ya nyonga sugu.
Uholanzi pia iko nchini ya amri ya kutotoka nje ambayo itaendelea kudumishwa hadi Januari 19.
Uturuki imeanza kutekeleza amri ya kutotoka nje kwa siku nne.

Virusi vya corona: Jinsi maradhi hayo yalivyovuruga sherehe za mwaka mpya duniani Virusi vya corona: Jinsi maradhi hayo yalivyovuruga sherehe za mwaka mpya duniani Reviewed by cmakigo on January 01, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.