UTAFITI: Mbuzi anavutiwa zaidi na binadamu anaetabasamu



Wanasayansi wamebaini kwamba mbuzi anavutiwa na binaadamu wanaotabasamu, Utafiti huo umeelezea kwa kina namna ambavyo wanyama huwa wanatambua hisia za watu zaidi ya ilivyokuwa inafikiriwa awali.

Watafiti wamewaonesha mbuzi picha za mtu mmoja, moja iliyomuonyesha akiwa amekasirika na nyingine mtu huyo akiwa na furaha.

Katika jarida la Open Science, watafiti wameeleza kwamba mbuzi hao walifanikiwa kuifuata picha ya mtu aliye na furaha. Matokeo hayo yanadhihirisha kwamba uwezo wa wanyama kutafsiri hisia za binadamu sio mdogo ikilinganishwa na mbuzi ambao wameishi na kufugwa kama mbwa au farasi.

Badala yake inaonekana kuwa wanyama wanaofugwa kwa chakula kama mbuzi pia wanaweza kutambua hisia usoni mwa binaadamu. Watafiti wamebaini kwamba mbuzi wanapenda zaidi watu wanaotabasamu na kuzifuata picha za watu wenye furaha kabla ya kutambua picha za watu waliokasirika, pia walitumia pua zao zaidi kuzitambua vizuri picha za watu wanaotabasamu.

Lakini picha hizo za muonekano wa furaha ziliwapendeza zaidi zilipowekwa katika upande wa kulia. Watafiti wanaamini huenda ni kwasababu mbuzi wanatumia upande wa kulia wa ubongo wao kutathmini matukio jambo linalodhihirika kwa wanyama wengine.

Na picha hizo zilipowekwa katika mkono wa kushoto mbuzi hao hawakuonekana kuvutiwa nazo, inaweza ikawa upande wa kushoto wa ubongo ndio unatafakari hisia chanya au upande wa kulia wa ubongo ambao hauonesha sura ya hasira.

Dr. McElligott kutoka chuo kikuu cha Roehampton anasema utafiti huu ni muhimu kwa sababu umeonyesha namna ambavyo mnyama anaweza kuhusiana na viumbe hai wengine kwa sababu uwezo wa mnyama kuelewa hisia za binaadamu huenda umesambaa na sio tu kwa wanyama wa kufugwa nyumbani.


UTAFITI: Mbuzi anavutiwa zaidi na binadamu anaetabasamu  UTAFITI: Mbuzi anavutiwa zaidi na binadamu anaetabasamu Reviewed by cmakigo on January 07, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.