Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu wamelaani shambulizi lililoendeshwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden nchini Yemen na kulitambua kuwa "kosa baya la jinai."
Katika taarifa iliyotolewa na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu, Katibu Mkuu Ali Muhyiddin al-Karadakh alisema, "Vitendo hivi ni dhambi na uhalifu kwa yeyote anayevifanya. Matukio haya yanastahili adhabu kali zaidi."
Akitoa wito wa kukomeshwa kwa vitendo vya kuhuzunisha na shida wanazopata wananchi wa Yemen, Karadakh alisisitiza kwamba kila mtu anapaswa kushiriki kutoa msaada wa maneno ya kibinadamu, kifedha, maadili na kisiasa ili kuiokoa Yemen kutokana na hali hii.
Wakati wajumbe wa baraza la mawaziri la serikali mpya ya Yemen walipowasili nchini hapo jana, milipuko 3 ilitokea katika kituo kimoja cha Uwanja wa ndege wa Aden.
Waziri wa Afya wa Yemen Kasim Buhaybeh alitoa maelezo kwenye akaunti yake ya Twitter na kutangaza kuwa watu 25 walipoteza maisha na wengine 110 walijeruhiwa kwenye milipuko hiyo iliyotokea katika uwanja wa ndege.
Waziri wa Habari na Utamaduni Muammar al-Iryani pia alitoa ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter na kusema, "Shambulizi hili la woga lililofanywa na wanamgambo wa Houthis wanaoungwa mkono na Iran kwenye Uwanja wa Ndege wa Aden halitatuzuia kutimiza wajibu wetu wa kitaifa."
Kwa upande mwingine, Mohammed al-Buhayti ambaye ni mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Houthis alisema, "Hatuna uhusiano wowote na shambulizi hilo."
Ulimwengu wa Kiislamu walaani shambulizi la Yemen
Reviewed by cmakigo
on
January 01, 2021
Rating:
No comments:
Post a Comment