Rais Museveni amemteua mwanajeshi kusimamia usalama wakati wa uchaguzi Uganda



Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemteua meja generali Kayanja Muhanga kuwa mratibu wa masuala ya usalama nchini Uganda .

Naibu msemaji wa jeshi luteni kanali Deo Akiiki ameambia BBC kwamba meja jenerali Muhanga atakuwa mratibu wa operesheni za vitengo vyote vya usalama.

‘Ni kweli kwamba Brigedia Kayanja Muhanga amepewa nafasi ya kuratibu vikundi vyote vya usalama kwa madhumuni ya kuunganisha shughuli ya usalama wa pamoja hususan katika mji wa Kampala na nchi yote’ .

"Hiyo ina maana kwamba atakuwa kiunganishi kati ya kikosi cha polisi , jeshi na idara ya ujasusi , alithibitisha luteni huyo.

Rais Museveni amemteua mwanajeshi kusimamia usalama wakati wa uchaguzi Uganda Rais Museveni amemteua mwanajeshi kusimamia usalama wakati wa uchaguzi Uganda Reviewed by cmakigo on January 06, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.