Mahakama ya Urusi yaagiza Navalny kusalia kizuizini

 


Mahakama nchini Urusi hii leo imeagiza kiongozi wa upinzani Alexei Navalny kuendelea kushikiliwa kizuizini hadi Februari 15, katika kikao cha kusikiliza madai dhidi yake kilichopangwa kwa dharura baada ya kukamatwa kwake. Wakili wa Navalny Vadim Kobzev aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kutokea kwenye chumba cha mahakama kilichojengwa kwa muda kwenye kituo cha polisi kwamba mahakama imeamua Navalny kuendelea kushikiliwa kwa siku 30 kuanzia siku ya Jumapili alipokamatwa. Awali, waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema Urusi haina uthibitisho wa madai yanayotolewa na mataifa ya magharibi kwamba kiongozi huyo wa upinzani alipewa sumu, zaidi ya ushahidi uliotolewa na yeye mwenyewe. Navalny alikamatwa jana alipokuwa anarejea kutoka Ujerumani alikokuwa akitibiwa kufuatia shambulizi la sumu, na kuituhumu Ikulu ya Kremlin kwa shambulizi hilo.

Mahakama ya Urusi yaagiza Navalny kusalia kizuizini Mahakama ya Urusi yaagiza Navalny kusalia kizuizini Reviewed by cmakigo on January 19, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.