Lady Gaga na Jennifer Lopez kutumbuiza wakati wa kuapishwa kwa
Jennifer Lopez na Lady Gaga walimuunga mkono Joe Biden katika kampeni za uchaguzi mwaka janaImage caption: Jennifer Lopez na Lady Gaga walimuunga mkono Joe Biden katika kampeni za uchaguzi mwaka jana
Lady Gaga alikampeni kwa alimfanyia kampeni Bw Biden wakti wa uchaguzi, ambapo alionekana nae katika mkesha wa siku ya uchaguzi mwezi Novemba mwaka jana.
Ataimba wimbo wa taifa katika sherehe za kuapishwa kwa Bw Biden tarehe 20 Januari. Lopez ambaye pia alimuunga mkono Bw Biden mwaka jana, atafanya onyesho la muziki siku hiyo.
Lady Gaga alijiunga na Biden katika kampeni siku moja kabla ya uchaguzi wa rais mwaka janaImage caption: Lady Gaga alijiunga na Biden katika kampeni siku moja kabla ya uchaguzi wa rais mwaka jana
Baada ya sherehe hizo, Tom Hanks ataonesha kipindi maalumu cha nyota wa muziki cha tevisheni.
Kipindi hicho maalumu kilichoitwa - Celebrating America, cha dakika 90 pia kitawashirikisha wanamuziki Warekani Jon Bon Jovi, Demi Lovato, Justin Timberlake na Ant Clemons, na kitatangazwa moja kwa moja katika vituo vya habari vya ABC, CBS, CNN, NBC and MSNBC.
Kamati ya maandalizi ya kuapishwa kwa Bw Biden imesema kuwa "itasherehekea mwanzo wa safari mpya ya taifa kuelekea umoja wa Marekani" na kuonesha uvumilivu, ushujaa na utashi wao wa kuungana na kuwa pamoja kama taifa katika kupona na kujijenga upya ".
No comments:
Post a Comment