KUFUGA SAMAKI KITALAAMU JIFUNZE UFUGAJI BORA WA SAMAKI

 


UTANGULIZI 

Ufugaji wa samaki unakua kwa kasi sana hapa nchini tanzania kutokana na kuonekana kua na faida sana. hivyo nimeamua leo nikupe elimu kidogo ambayo itakusaidia wewe mfugaji ambaye ungependa kujikita katika ufugaji huo, hivyo tue pamoja ili kujua mengi. 


SIFA ZA ENEO LA KUFUGIA SAMAKI 

Sio kila mahali hufaa kwa ufugaji wa samaki, ila mahali ambapo ni sahihi, zifuatazo ni sifa za eneo bora la kufugia samaki. 

eneo linalo fikika kwa urahisi 

eneo tulivu na lenye usalama wa kutosha 

eneo ambalo linavibali vyote vya umiliki 

lazima liwe na maji ya kutosha kwa kipindi chote utakacho fuga 

eneo ambalo halina mmomonyoko wala historia ya mafuriko 

eneo lenye uwezo wa kutuamisha maji 

eneo ambalo soko lake sio la shida 

UTENGENEZAJI WA BWAWA 

Kuna aina mbali mbali za kutengeneza mabwawa ya samaki inategemea na eneo, kiasi cha samaki unao taka kufuga, aina ya samaki na hali ya uchumi. 


aina hizo ni 

bwawa la kuchimba udongo bila kujengea(earthen pond) 


bwawa la kuchimba na kujengea 

hivyo unaweza kuchangua kulingana na sifa nilizo taja hapo mwanzo 

UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA/MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA 

Kabla vifaranga hawaja safirishwa ni vyema kuwatoa katika bwa kubwa wanalo ishi na kuwaweka katika vibwa vidogo vidogo kati ya masaa 24 hadi 72 kuendana na umbali wa safari bila kuwapa chakula chochote kile. 

baada ya kuwasafirisha mfugaji atakiwi kuviweka kwenye bwa moja kwa moja ila inatakiwa maji yalio tumika katika kuwasafirisha yabadilishane joto na maji ya bwawa ambalo wataenda kuishi. hivyo mfugaji anatakiwa kuliweka kontena ambalo vifaranga wamo ndani ya bwawa ambalo wataishi kwa dakika 30 hadi 35 bila kuwafungulia, baada ya hapo kontena liina mishwe taratibu ili kuwezesha maji ya bwawa na yaliyo kwenye kontena kubadilishana na baadae vifaranga watatoka taratibu, 

endapo hautafanya hivyo unaweza kusababisha vifaranga vyote kufa kutokana na mabadiliko ya joto ambayo yanaweza kutokea ghafla. 

unatakiwa kusafirisha vifaranga wako mda ambao hali ya hewa inakua sio joto yaan mda wa jion na asubuhi ili kuwezesha vifaranga kuimili misukosuko ya safari na bila kupatwa na joto kali. 

CHAKULA NA UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI 

Samaki hutakiwa kupewa chakula angalau mara 2 kila siku unatakiwa kuzingatia mda sahihi wa kuwapa chakula yaan asubuhi saa 3-4 na jion saa 9 -10 samaki upewa vyakula tofauti kulingana na aina. 

tabia ya ulaji wa samaki ni kama ifuatavyo 

samaki wanao kula nyama (sangara, kambale) 

samaki wanao kula mimea carps 

samaki wanao kula mchanganyiko (perege,sato na samaki wa maji ya chumvi mfano kibua) 

zingatia kuweka maji ambayo ni safi 

TARATIBU ZA ULISHAJI WA SAMAKI 

UMRI(wiki) UZITO(gm) KIASI CHA CHAKULA KWA SIKU (gm)

(Umri)    (Chakula)     (Uzito)

1-2            5-10            1 

2-3            20-50          2 

3-5.           50-110        3 

5-7.            110-200     4

7 nakuendelea 200 na zaidi


KUFUGA SAMAKI KITALAAMU JIFUNZE UFUGAJI BORA WA SAMAKI KUFUGA SAMAKI KITALAAMU  JIFUNZE UFUGAJI BORA WA SAMAKI Reviewed by cmakigo on January 27, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.