Kiasi ya watu 56 wauawa katika shambulizi la Niger



Watu waliokuwa na silaha wamewauwa kiasi ya raia 56 na kuwajeruhi zaidi ya 20 katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la kigaidi nchini Niger. 

Waziri wa Mambo ya Ndani Alkache Alhada amesema shambulizi hilo lilitokea katika vijiji vya Tchombangou na Zaroumdareye karibu na mpaka na Mali. 

Maelezo zaidi kuhusu shambulizi hilo hayajatolewa. 

Shambulizi hilo limetokea wakati Niger ikihesabu kura za uchaguzi wa Desemba 27. Mpaka jana, matokeo yaliyotangazwa yanaonyesha chama tawala cha Demokrasia na Ujamaa kinaongoza viti vya bunge. 

Uchaguzi wa rais utaingia katika duru ya pili mwezi Februari baada ya kutopatikana mshindi wa moja kwa moja. 

Mgombea wa chama tawala Mohamed Bazoum alipata asilimia 39.6 ya kura na mgombea wa upinzani Mahamane Ousmane akipata asilimia 16.9. 

Taifa hilo linatarajiwa kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru mwaka 1960 kutoka Ufaransa, kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia

Kiasi ya watu 56 wauawa katika shambulizi la Niger Kiasi ya watu 56 wauawa katika shambulizi la Niger Reviewed by cmakigo on January 03, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.