Ni maswali huulizwa na wengi na kila mtu hutaka kujua je, matajiri duniani ni akina nani. Kuna watu wengi sana wenye wako na hela ndefu sana na hata wakati mwingine hukopesha hata nchi zao. Kwa sasa tunajaribu kutoa orodha fupi ya watu matajiri duniani.
Jeff Bezos
Kama wewe hupenda kununua bidhaa kwa mitandao basi utakuwa umekutana na kampuni ya Amazon. Kampuni hii inamilikiwa na Jeff Bezos. Jeff ndiye anasemekana kuwa tajiri duniani kwani utajiri wake ni kimo cha dola bilioni $145. Jeff Bezos pia anamiliki gazeti moja la marekani kwa jina Washghton post. Kama pia ushawahi kusikia mambo na Space technology basi ujue kuwa Jeff Bezos amewekeza sana kwa hii teckinologia.
Bill Gates.
Ni mwanzilishi wa Microsoft na ni tajiri zaidi duniani. Forbes ilimueka kwenye orodha ya matajiri kwa miaka mingi. Bill gates ako na taasisi yake ama ukipenda Foundation yake kwa jina Bill and Melida gates foundation. Utajiri wake ni dola bilioni 106.6.
Bernard Arnault.
Ni mzaliwa wa ufarasansa na kwa sasa ako kwa orodha ya watu matajiri duniani. Kama unapenda kuvaa nguo za kampuni ya luis Vuitton na Sephora, basi elewa zinatengenezwa na kampuni yake benard Arnault. Balani ulaya, tajiri huyu ameshikilia nambari ya kwanza ila dunia nzima anashikilia nafasi ya tatu. Utajiri wake ni dola bilioni 91.6
Mark Zuckerberg
Ni mmiliki wa mitandao kadhaa ikiwemo facebook, Whatsapp na Instagram. Kama unatumia kati ya mitandao niliyoitaja basi jua kuwa zinamilikiwa na Mark Zuckerberg. Ni tajiri mwenye umri mdogo sana kwani alianzisha facebook mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka kumi na tisa. Utajiri wake kwa sasa ni dola bilioni 78.6
Wallen Buffett
Wallen buffett ni kati ya watu majiri zaidi duniani. Tajiri huyu anamiliki kampuni ya berkshire hathaway. Wallen buffett hutoa msaada zaidi kwa wasiojiweza na ni juzi tu aliahidi kugawa asilimia tisaini ya utajiri wake kwa watu wasiojiweza. Kwa miongo tisa, Tajiri huyu hajawahi kosa kwenye orodha ya watu matajiri duniani. Utajiri wake kwa sasa ni dola bilioni 68.8
Steve Ballmer
Steve ballmer aliwahi kuwa mkurugenzi wa microsoft kati ya mwaka 2000 hadi 2014. Alianza kufanyia kazi kampuni hiyo tangia 1980. Kabla ya kujiunga na kampuni ya microsoft, tajiri huyu alikuwa chuo kikuu cha stanford ambapo alikuwa anasomea shahada ya uzamili. Hakuweza kumaliza shahada hiyo baada ya kupata nafasi ya kazi ndani ya kampuni ya microsoft. Baada ya kuacha kazi ndani ya microsoft, Steve Ballmer alinunua klabu ya mpira wa vikapu ya Los angeles clippers. Utajiri wa Steve Ballmer ni dola bilioni 66.4
Larry Page.
Ni mmoja kati ya wanzilishi wa kampuni ya Google. Kumbuka tajiri mwingine aliyehusika na uanzilishi wa kampuni ya google ni Sergey Brin. Kampuni ya Google ilianzishwa mwaka wa 1998. Mwaka wa 2019, Larry Page alijitoa uongozini wa kampuni ya Alphabet ingawa bado ni mmoja wa bodi ya kampuni hiyo. Utajiri wa Larry Page kwa sasa ni dola bilioni 63.3.
Sergey Brin
Sergey brin na Larry Page ndio walioanzisha kampuni ya Google. Yeye pia aliamua kuachana na ka alphabet mwaka wa 2019. Kwa sasa anatumia mda wake mwingi kwa utafiti bila kusahau yeye bado ni mjumbe wa bodi ya Alphabet. Utajiri wa Sergey Brin ni dola bilioni 61
No comments:
Post a Comment