Assange kuijua hatma yake leo

 


Mwasisi wa mtandao wa ufichuzi wa taarifa za siri wa Wikileaks Julian Assange atajua leo uamuzi wa mahakama ya Uingereza, juu ya ikiwa atasafirishwa kwenda Marekani kukabiliwa na mashitaka ambayo ni pamoja na uhalifu wa kijasusi na kuchapisha nyaraka za siri za jeshi la Marekani. 

Assange ambaye ni mzaliwa wa Australia anatuhumiwa kudukua kompyuta za serikali ya Marekani na kuvunja sheria ya nyaraka nyeti kwa kuweka hadharani marundo ya mafaili ya siri ya kijeshi na kidiplomasia. 

Ikiwa mahakama hiyo ya Uingereza itaamua apelekwe Marekani, na ikiwa atapatikana na hatia kwa mashitaka hayo, Assange mwenye umri wa miaka 49 anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka kati ya 30 na 40 jela, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa mawakili wake.


Assange kuijua hatma yake leo Assange kuijua hatma yake leo Reviewed by cmakigo on January 04, 2021 Rating: 5

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();
Powered by Blogger.